TMDA yataja sifa kutambua vitakasa mikono bora

0
116

Watanzania wametakiwa kuepuka vitakasa mikono (senitizer) ambavyo havijathibitishwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) ili kuepuka madhara.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mchunguzi wa Maabara ya TMDA, Gerald Sambu amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa bidhaa hiyo, baadhi ya wafanyabishara wametengeneza vitakasa mikono visivyokuwa na ubora kwa afya.

“Ili kuepuka athari hizo ni vyema kila mtu anapoenda kununua vitakasa mikono akawa makini kujiridhisha kama vimesajiliwa na TMDA,” Gerald Sambu.

Amesema wananchi wanatakiwa kuzingatia tarehe ya kumalizika matumizi kwa vitakasa mikono jambo ambalo linaweza kuwaepusha kutumia senitizer zilizopitwa na muda.

Sambu ametaja sifa za vitakasa mikono vizuri kuwa ni vile visivyowahi kukauka au kuchelewa kukauka mikononi baada ya kupaka, vyenye kipimo cha kutambua kiwango cha asidi na besi (PH 6-8), hivyo ikiwa chini ya hapo au kuzidi haifai kwa matumizi.

Amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) vitakasa mikono bora ni vile vilivyotengenezwa kwa kutumia kilevi ingawa vingine vinatumia kemikali.