Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imesema kuwa inafanya utafiti wa Dawa za nguvu za kiume aina ya Viagra kwa kuangalia matumizi yake kwa ukubwa na yapo kwa kiasi gani ili waweze kutoa elimu sahihi kwa jamii.
Mkurugenzi wa mkuu wa TMDA, Adam Fimbo amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba.
Fimbo amesema wananchi wanapaswa kufuata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizo.