TMA yatangaza ongezeko la mvua baadhi ya mikoa

0
2459

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini –TMA, imetangaza kuwepo kwa ongezeko la mvua katika kipindi cha kuanzia Novemba 2018 hadi Aprili 2019 na kuwataka wadau wa sekta mbalimbali  kuchukua tahadhari.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi ametoa tahadhari hiyo jijini Dar Es Salaam wakati akielezea mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata mvua za msimu mmoja huku akiainisha maeneo yatakayokumbwa na mvua hizo.

Amewataka wadau mbalimbali kuchukua tahadhari ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wingi wa mvua.

Maeneo yatakayokumbwa na mvua hizo ni pamoja na Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini Magharibi na Kusini mwa nchi, Ukanda wa Pwani ya Kusini na maeneo yaliyo Kusini mwa mkoa wa Morogoro.