Watu TISA wamefikishwa kizimbani kwa tuhuma za uhujumu uchumi na kuingizia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 5.8 Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar Es Salaam watuhumiwa wamesomewa mashtaka KUMI yanayowakabili katika kesi ya uhujumu uchumi namba 20 ya mwaka 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shaidi.
Washtakiwa hao wanatuhumiwa kuendesha mtandao wa uhalifu ikiwemo kusajili masafa kinyume na kanuni za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka, Biswalo Mganga ametoa wito kwa wawekezaji nchini kuzingatia sheria na kwamba ofisi yake itakuwa macho kumulika wavunja sheria na kuchukua hatua