Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) leo tarehe 26/7/2022 imefanya kikao na Melinda Taylor, ambaye ni Makamu wa Rais wa Shirika la International Education.
Katika Mkutano huo Melinda Tylor ambaye aliwahi kuwa mke wa Bill Gates, amesema kuwa amefurahishwa na namna Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ilivyoshirikiana na RTI International katika kutekeleza miradi ya TUSOME PAMOJA na JIFUNZE UELEWE.
Makamu huyo wa Rais ameahidi kuongeza wigo wa ushirikiano katika masuala mbalimbali yakiwemo mafunzo kazini kwa walimu na utafiti.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba amesema kuwa wapo tayari kushirikiana katika maeneo hayo ya utafiti na utoaji wa mafunzo kazini kwa walimu na kuwa ushirikiano huo utasaidia kuboresha ufundishaji na ujifunzaji shuleni.
Amemuomba Makamu huyo wa Rais kuangalia uwezekano wa kupanua wigo wa utekelezaji wa miradi ya JIFUNZE UELEWE na TUSOME PAMOJA ili iwafikie walimu na wanafunzi wote nchini.