Tenga alia na umri wa wachezaji Afrika

0
384

https://www.youtube.com/watch?v=S3b7zXaAadg&feature=youtu.be

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF)  – Leodgar Tenga amesema kuwa udanganyifu wa umri unaofanywa na wanasoka wa Bara la Afrika unasababisha kukosekana kwa maendeleo endelevu kwenye mchezo huo.

Tenga ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya ndani ya maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana walio na umri wa chini ya miaka 17 (AFCON-U17)  zilizomalizika hivi karibuni nchini Tanzania amesema kuwa,  ili kuondokana na tatizo hilo kuna umuhimu wa kuwa na dhamira ya dhati ya kuendeleza soka na siyo kuangalia mafanikio ya muda mfupi.

Baadhi ya makocha wa timu zilizoshiriki Fainali hizo walilalamikia udanganyifu wa umri kwa baadhi ya wachezaji walioshiriki,  jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu hasa kwa wachezaji wa Afrika wanaocheza soka la kulipwa Barani Ulaya na Mataifa yaliyoendelea.