TEMESA: Utengenezaji wa magari ya serikali kuchukua muda mfupi

0
239

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Ma wasiliano, Mhandisi Elias Mwakalinga amezindua vitendea kazi mbalimbali vitakavyosambazwa kwenye karakana 14 za Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

Akizindua vitendea kazi hivyo Mhandisi Mwakalinga amesema vifaa hivyo vitasaidia kuleta matokeo chanya ya fedha za Serikali.

Pia, ameongeza kuwa kazi kubwa ya wizara ni kuwezesha wakala kutimiza majukumu yake hivyo kuwataka watendaji wa TEMESA kutunza vifaa hivyo viweze kuleta tija kwa watumishi wa umma.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TEMESA, Sylvester Semfuko ameishukuru serikali kwa kuwezesha ununuzi wa vifaa hivyo nakubainisha kuwa vitasaidia kuharakisha utengenezaji wa magari ya serikali yanayochukua muda mrefu yakiwa karakana.