Televisheni ya Kiingereza kujenga taswira chanya ya Tanzania

0
240

Shirika la utangazaji Tanzania (TBC) linakaribia kuanzisha televisheni ya Kiingereza ambayo itaanzia mtandaoni kutokana na uhitaji wa kuitangaza na kuijengea taswira chanya ya Tanzania ndani na nje ya mipaka.

Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba Chacha ametoa kauli hiyo hii leo katika mahojiano maalamu na kipindi cha Jambo Tanzania ambapo alikuwa akianisha mipango ya shirika la hilo kwa mwaka 2022.

” Lazima tuwe na channel ambayo itakuwa inaeleza matukio ya hapa nchini, ya Afrika na duniani kwa mtazamo wetu sisi wenyewe”. Amesisitiza Dkt. Rioba.

Mapema Dkt. Rioba ameainisha Kuwa TBC ni kituo pekee cha habari nchini chenye jukimu la kulinda tamaduni mbali na majukumu mengine ya msingi ya kituo cha habari .

Pia amesisitiza Kuwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) litajikita zaidi katika mitandao ya kijamii ikiwa ni hatua muhimu katika kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha Watanzania.