Teknolojia nyenzo ya biashara ya usafirishaji binadamu

0
128

Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na mapambano dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu (TATLI) limesema, matumizi mabaya ya teknolojia yamekuwa nyenzo ya kufanikisha biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.

Mkurugenzi wa
TATLI Godfrey Mpandikizi ameitaja mitandao ya kijamii kuwa moja ya nyenzo hizo.

Mpandikizi alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam, wakati akitoa ripoti ya nusu mwaka 2022 juu ya tathmini ya mapambano dhidi ya biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.

Amesema ripoti kadhaa zimeitaja Tanzania kuwa ni moja ya nchi zinazoongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwa na matukio mengi ya biashara haramu ya kusafirisha watoto.

Akizungumzia maadhisho ya siku ya biashara haramu ya usafirishaji binadamu duniani yanayotarajiwa kufikia kilele chake Julai 30 mwaka huu, Mpandikizi
amesema Umoja wa Mataifa ulianzisha siku hiyo kwa lengo la kutoa elimu na kuhamasisha jamii kupinga biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.