TEHAMA kuwa mjadala mkuu Mkutano wa Jeshi la Polisi

0
125

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema dhima ya mkutano uliozinduliwa hii leo na Rais Samia Suluhu Hassan ni TEHAMA, ikilenga kuimarisha uwazi na uwajibikaji.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam katika ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Polisi, Waziri Masauni amesema mbali na Jeshi hilo kuibua mifumo ya TEHAMA 13 ili kuongeza ufanisi katika majukumu ya Jeshi hilo ili kuepusha changamoto na kero kwa Wananchi, matumizi ya mifumo hiyo hayaepukiki.

Hata hivyo Masauni ameongeza kuwa kutokana na umuhimu huo, ajira zilizotolewa za Jeshi la Polisi zimetumika kupata askari wa Jeshi hilo wenye taaluma ya TEHAMA takribani 80 ili wasimamie mifumo hiyo.

Waziri Masauni ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Nchini linaendelea kushirikiana na Mashirika ya uzalishaji Mali ambapo Jeshi hilo hivi sasa limefanikiwa kushirikiana na taasisi mbalimbali kuibua miradi kadhaa.

Ametaja moja ya miradi hiyo kuwa ni ule wa Miji Salama ambao utaanza siku za usoni na kwamba hadi sasa kwa nchi za Afrika Mashariki ikiwa sio nchi chache basi huenda mradi huo ukawa unapatikana hapa nchini pekee.