TEA yazidi Kuboresha miundombinu ya Elimu

0
319

Mamalaka ya Elimu Tanzania (TEA) Imeendelea kuboresha miundombinu ya Elimu Jijini Dodoma kwa kuwezesha ukarabati na upanuzi wa shule nne za msingi.

Katika ufuatiliaji wa miradi mbalimbali inatotekelezwa na TEA, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Prof. Maurice Mbago ametembelea mradi wa utanuzi na ukarabati wa shule nne za Msingi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofadhiliwa na TEA na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo uliogharimu Shilingi Bilioni 1.9.

Katika ziara hiyo ya siku moja Prof. Mbago, ametembelea shule ya msingi Medeli na Kisasa ambazo ni miongoni mwa shule nne zilizofadhiliwa na TEA.
Shule nyingine zilizifadhiliwa ni Mlimwa C na Kizota.

Waalimu wakuu wa shule za Msingi Medeli Bi. Grace Lisasi na shule ya Msingi Kisasa Bi. Jesca Mwarabu wamesema mradi huo umesaidia kuongeza ufaulu na udahili wa wanafunzi

Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amepongeza TEA kwa ufadhili huo ambao amesema umeboresha mwonekano miundombinu na mandhari za shule nufaika

Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bahati Geuzye amehimiza wanufaika wa mradi huo kutunza vizuri miundombinu hiyo kwa manufaa ya watanzania