TCU yafungua dirisha la pili la udahili

0
170

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Profesa Charles Kihampa amesema jumla ya waombaji 86,624 kati ya waombaji 116,133 sawa na asilimia 74.6 wamepata nafasi ya kujiunga na vyuo walivyoomba kwa mwaka wa masomo 2023/2024.

Profesa Kihampa amesema awamu ya kwanza ya udahili imefungwa, lakini wamefungua dirisha la pili kwa waombaji wengine kufanya hivyo kupitia katika vyuo wanavyotaka kujiunga.

Aidha, TCU imewataka waombaji wote waliodahiliwa kwenye chuo zaidi ya kimoja kufanya uthibitisho katika chuo kimojawapo kwa mawasiliano maalum na chuo husika.

Jumla ya waombaji 43,213 wamedahiliwa chuo zaidi ya kimoja kwa mwaka wa masomo 2023/2024 na mwisho wa kuomba na kuthibitisha ni Septemba 06,2023.