Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ameliambia Bunge kuwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limeboresha maudhi yanayorushwa kwenye redio, televisheni na mitandao ya kijamii.
Waziri Nape amesema ubunifu huo wa kimaudhui na uwasilishaji umeongeza mvuto kwa vyombo vya habari vya TBC.
Ameongeza kuwa TBC ilifanikiwa kununua haki za kutangaza michuano ya Kombe la FIFA la Dunia ambapo jumla ya michezo 28 ilirushwa TBC1 na michezo yote 64 ilirushwa TBC Taifa na TBC Online.
Akiwasilisha bajeti ya wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habarin kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 Bungeni jijini Dodoma Waziri Nape amesema, uanzishwaji wa kurusha taarifa ya habari kwa lugha ya Kiingereza umeanza mwezi Novemba mwaka 2022 na hivyo kupanua wigo wa habari zinazotangazwa na shirika hilo.