TBC yapewa kongole kwa ushirikiano mzuri na Chuo Kikuu cha Iringa

0
358

Chuo Kikuu cha Iringa kimelipongeza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuwapokea, kuwalea na kuwakuza wahitimu wa tasnia ya habari kutoka chuoni hapo.

Chuo hicho kimetoa pongezi hizo leo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba Chacha wakati wa mahafali chuoni hapo na kueleza kuwa licha ya soko la ushindani, TBC imeendelea kufungua mikono yake kuwapokea na kuwapa nafasi wahitimu wa tasnia hiyo.

Aidha, wamempongeza Dkt. Rioba na kumwambia “Umekua nuru kwa tasnia ya habari na kuweka tumaini jema kwa wahitimu wetu ambao tunajivunia.”

Wahitimu wa chuo hicho ambao ni watendaji wa TBC ni pamoja na Anna Mwasyoke, David Charles, Essero Mafuru, Ezekiel Simbeye, Henry Mbilinyi, Irene Mwakalinga, Khalid Nziva na Oscar Urassa.