TBC yaleta mapinduzi makubwa katika upashanaji habari

0
311
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwekyembe (katikati) akiwa ndani ya studio mpya ya TBC pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba (Kulia), ikiwa ni studio itakayotumika kwa ajili ya #TBCAridhio.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe leo ameweka jiwe la msingi la uzinduzi wa studio mpya za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), hafla iliyofanyika katika viwanja vya shirika hilo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mwonekano Mpya wa TBC

Mbali na uzinduzi wa studio, katika hafla hiyo Waziri Mwakyembe pia amezindua programu tumishi (App) ya Safari Channel, pamoja na kuzindua mfumo mpya wa upashanaji habari unaofahamika kama TBC Aridhio.

TBC inakuja na mabadiliko haya makubwa ya upashanaji habari baada ya miaka 13, ambapo safari hii ilianza mwaka 2007.

Ujenzi wa jengo hilo la kisasa ulioanza Februari 2020 utagharimu shilingi bilioni 2.38, na unatarajiwa kukamilika Agosti 2020, ambapo hadi sasa ujenzi huo umefikia asilimia 20.