Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameliagiza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupitia bodi yake kuhakikisha linaweka uzio eneo la ekari zaidi ya 67 lenye mitambo ya analogia, lililopo Iwambi mkoani Mbeya, ili kuepusha uvamizi.
Waziri Nape amezungumza hayo mara baada ya kutembelea viwanja hivyo ambavyo kumekuwa na uwekezaji wa mitambo ya radio ambapo sehemu ya eneo linadaiwa kuvamiwa na baadhi ya watu.