TBC kutoa tuzo kwa wasanii

0
160

Katika kuhakikisha linaenzi na kuthamini kazi za wasanii, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), litaanza kutoa tuzo kwa wasanii wakongwe na kizazi kipya kwa lengo la kutambua mchango wao katika jamii kupitia sanaa.

Hayo ameyaeleza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt. Ayub Rioba katika kipindi cha Jambo Tanzania, wakati akifananua kuhusu tamasha la Tukutane Kwetu litakalofanyika Mei 21 mwaka huu.

“Sisi TBC ndio baba wa sanaa, tumeanza kupiga nyimbo za wasanii miaka ya nyuma kabisa, hivyo lazima tuwapongeze kwa kazi wanazofanya na hii si kwa wakongwe tu hata hawa wapya, lengo ni kutambua mchango wao katika sanaa”-amesema Dkt. Rioba

Mei 21 mwaka huu kutakuwa na tamasha la Tukutane Kwetu litakalowakutanisha wasanii wote nchini, tamasha hilo litafanyika katika ofisi za TBC zilizopo Mikocheni, Dar es Salaam.