TBC kusikika nchini nzima ndani ya mwaka mmoja

0
432

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kwamba Serikali imeimarisha usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambapo mpaka sasa usikivu ni zaidi ya asilimia 70 na matarajio ni kufikia maeneo yote ndani ya mwaka huu wa fedha.

Kwa upande wake Mhandisi Mkuu wa Shirika hilo, Upendo Mbelle amesema katika kuimarisha usikivu wa TBC mkoani Morogoro shirika linajenga kituo eneo la Kisaki na kuweka mtambo wa kilowati moja (KW 1) ambacho kikikamilika mkoa wote utasikika, huku akeleza kuwa eneo la Mlimba litawekwa mtambo ambao tayari umeshaagizwa na mkandarasi ameanza kufanya kazi.

“Morogoro ina changamoto ya milima na mabonde, lakini tukimaliza kuweka mitambo katika maeneo hayo usikivu hautakuwa na shida tena, na baada ya kazi hiyo tutafunga mtambo mdogo katika Wilaya ya Gairo”, amesema Mbele.

Vilevile, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Olesanare amesema mkoa huo unafanya vizuri katika sekta zote za wizara hiyo ikiwemo kuhifadhi na kulinda mila na desturi pamoja na kulinda maeneo yote ya kiutamaduni yalipo mkoani hapo.