TBC kuendelea kuwafikia watu wengi zaidi

0
195

Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema TBC imeendelea kuboresha usikivu wa radio ili ifike hadi maeneo mengi ya vijijini na kuwahabarisha Watanzania juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo na shughuli za kijamii.

Dkt. Rioba amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mkutano 106 wa mafunzo ya uandaaji wa vipindi vya televisheni, redio na mitandao ya kijamii kwa maofisa wa habari wa wizara, taasisi, mashirika ya umma, idara na halmashauli mkoani Iringa yaliyozinduliwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerison Msigwa.

Aidha, amesema TBC ina mpango wa kuanzisha chaneli ya lugha ya Kiingereza kwa lengo la kuwawezesha hata watu wasiofahamu Kiswahili wajue mambo mbalimbali yanayoendelea nchini ikiwepo kufikisha ujumbe kwa watu wa mataifa mabalimbali.

Amewashukuru wadhamini wa mkutano huo kwa kujitoa kwao na kurahisisha mafunzo kwa washiriki na kuamini kuwa washiriki watafanya vizuri kwenye uandaaji wa vipindi vya elimu kwa umma.

TBC imeandaaa mkutano wa 106 wa mafunzo ya uandaaji wa vipindi vya vya televisheni, redio na mitandao ya kijamii mkoani Iringa ambayo yanatolewa kwa maofisa wa habari wa serikali.