TASAF kuzifikia kaya masikini kielektroniki

0
140

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), ambao hutoa huduma kwa kaya masikini umekuja na mfumo mpya wa kufikisha fedha kwa walengwa kwa njia ya kielektroniki.

TASAF imekuja na mfumo huo kwa lengo la kumfikia mlengwa kwa urahisi na usalama zaidi kwa njia ya benki au simu ya mkononi.

Akizungumza katika mafunzo ya kujenga uelewa kwa wawezeshaji kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza, Zakaria Msomi ambaye ni Afisa wa Malipo kwa njia ya mtandao amesema mfumo huo unamsaidia mlengwa kutimiza malengo yake kwa kuhifadhi fedha benki na kutotumia fedha bila malengo na matarajio.