TARURA yashusha neema ya barabara Arusha

0
255

Wawekezaji na wananchi Mkoani Arusha wamemsifu na wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwajengea kwa kiwango cha lami barabara za Themi -Viwandani zenye urefu wa kilometa 1.4 kwagharama ya shiligi 1,175,141,850.00.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja jijini Arusha iliyofaywa na bodi ya ushauri ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA).

“Wageni walikuwa wakija eneo la Kiwanda na kuona miundombinu mibovu walikuwa wanapata wasiwasi na kiwanda pia, lakini tumeona Serikali yetu imeona changamoto na kuifanyia kazi haraka, sasa tunaaminika kwa sababu mazigira yameboreshwa,”

Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo, amewashukuru watendaji na wataalamu wa TARURA kwa kazi kubwa inayofanywa na serikali.

“Huko nyuma kaba ya kuanzishwa TARURA ilikuwa ngumu kupeleka mradi sehemu inayoeleweka na ukaleta tija kwa sababu kila diwani alikuwa akivutia upandewa wake. Leo mmewasikia hapa wawekezaji wamesubiri barabara kwa takribani miaka 40 lakini baada ya TARURA kuanzishwa barabara imejengwa,’amesema Gambo.

Mtendaji mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff amesema kuwa wamejipanga kuwafikia wannachi katika sehemu ambazo hazifikiki na pia katika maeneo ya kimkakati.