Tanzia: Mwandishi wa TBC, Elisha Elia afariki dunia

0
545

Aliyekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Elisha Elia amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba imesema Elia amefariki jioni leo Oktoba 24, 2020.

Taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu zitatolewa hapo baadaye.