Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha anasikitika kutangaza kifo cha mwandishi wa habari mwandamizi wa TBC, Marin Hassan Marin kilichotokea leo asubuhi jijini Dar es Salaam.
Mipango ya mazishi inaendelea kufanywa.
Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.