TANZIA : MFUGALE AFARIKI DUNIA

0
184

Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale afariki dunia leo Tarehe 29 Juni, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma baada ya kuugua ghafla majira ya saa 5 asubuhi.

Mbali na barabara, enzi za uhai wake Mfugale alisimamia ujenzi wa madaraja mbalimbali ikiwa ni pamoja na Daraja la Mkapa kwenye mto Rufiji, Daraja la Rusumo katika Mto Kagera, Daraja la Kikwete, kwenye mto Malagarasi, Daraja la Nyerere, Kigamboni, Daraja la Mfugale na Daraja la Kijazi mkoani Dar es Salaam.

Mfugale aliteuliwa kushika wadhifa huo Mei 2011.

Kabla ya uteuzi huo alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS na aliwahi kushika nafasi mbalimbali katika serikali na kusimamia ujenzi wa barabara na madaraja muhimu kwa taifa.

Aidha, Mfugale pia aliwahi kushika majukumu maalumu katika wizara ya ujenzi kama Mkurugenzi wa Idara ya Barabara za Mikoa.

Mfugale alikuwa na Shahada ya Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Roorkee India, na Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu Loughborough cha Uingereza, ni mhandisi alisajiliwa na alihudhuria mafunzo ya Ujenzi na uchumi, Mafunzo ya miradi na utunzaji wa barabara pamoja na ujenzi na utunzaji wa madaraja.