Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile amefariki dunia katika Hospitali ya Regency usiku wa kuamkia leo February 20,2021 baada ya kuugua kwa muda mfupi, Mke wa Marehemu Likwelile, Mbunge Mstaafu Vicky Kamata amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Wakati wa uhai wake Dkt. Likwelile amewahi kuwa katibu mkuu wa wizara ya fedha na Serikali mpaka mwaka 2016.