Tanzania, Qatar kuimarisha ushirikiano

0
118

Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa Taifa la Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani huko Doha.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Oktoba 4, 2022, Rais Samia na mwenyeji wake wamezungumzia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano na biashara baina ya Tanzania na Qatar.