Tanzania yazindua filamu mahususi ya kutangaza utalii

0
354

Waziri wa Maliasili na utalii Dkt. Hamis Kigwangala amewaomba watanzania kusambaza mitandaoni na kwa njia nyingine filamu hiyo ya utalii ambayo imelenga kutangaza utalii wa Tanzania ili kuwafikia watu wengi ulimwenguni

Kigwangala amesema hayo wakati akizindua filamu hiyo jijini Dar es salaam huku akiwahakikishia watalii kuwa tahadhari zote zimewekwa kwaajili ya Corona.

Devota Mdachi mkurugenzi mwendeshaji bodi ya utalii Tanzania amesema filamu hiyo imetafsiriwa kwa lugha mbalimbali ili kuwafikia watalii wengi zaidi.

Hivi karibuni Rais John Magufuli alitangaza kufunguliwa kwa huduma za utalii hapa nchini baada ya kufungwa kwa muda kutokana na janga la Corona.