Tanzania yawasilisha ujumbe maalum kwa Marekani

0
275

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amewasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais John Magufuli kwenda kwa Rais Donald Trump wa Marekani, kupitia wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo.
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye pia anashughulikia masuala ya Afrika, -Tibor Nagy ndiye aliyepokea ujumbe huo jijini Washington na kuahidi kuendeleza ushirikiano mzuri na wa muda mrefu  uliopo kati ya Tanzania na Marekani.