Serikali ya Tanzania imesitisha safari zake za ndege kwenda nchini Afrika Kusini kutokana na vurugu zinazoendelea nchini humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa safari hizo zimesitishwa kwa muda hadi hapo serikali ya Afrika Kusini itakapothibitisha kwa maandishi juu ya usalama wa abiria na vyombo vya usafiri vitakavyoingia nchini humo.
Vurugu zimeendelea kwa siku kadhaa katika maeneo mbalimbali nchini Afrika Kusini ambapo baadhi ya Raia wa nchi hiyo wamekua wakiwashambulia wageni ambao wanafanya shughuli mbalimbali nchini humo pamoja na kuharibu mali zao.