Tanzania yaridhia Burundi kujiunga SADC

0
207

Serikali ya Tanzania imesema ipo pamoja na serikali ya Burundi katika harakati zake za kuomba kujiunga na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Akizungumza wakati wa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya ushirikiano baina ya Tanzania na Burundi mkoani Kigoma, Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wa kindugu baina ya nchi hizo.

Aidha, ameongeza kuwa njia pekee ya kuwaenzi waasisi wa mataifa hayo ni kuimarisha uhusiano katika nyaja za kiuchumi, kijamii pamoja na kudumisha usalama.