Tanzania yapokea ugeni mzito kutoka China

0
166

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, -Wang Yi amewasili  nchini hii leo  kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo amezindua Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) cha wilaya ya  Chato mkoani Geita.

Akizindua Chuo hicho Wang Yi amesema kuwa China itaendelea kuisaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyuo vya mafunzo ya ufundi.

Amesema China pia inasaidia kujenga chuo cha Ufundi Stadi cha Kagera ambapo kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya Wanafunzi elfu Moja.

Waziri huyo  wa Mambo ya Nje ya China amewasilisha msaada wa zaidi ya shilingi milioni 350 kwa ajili ya Chuo hicho cha VETA,  fedha ambazo zitatumika kununulia vifaa vya mafunzo.

Akitoa salamu za shukrani, Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt  Medard Kalemani amesema kuwa chuo hicho kitatunzwa na kuendelezwa kwa manufaa ya wananchi wa Chato na Tanzania kwa ujumla.