Tanzania yapinga matumizi ya silaha za nyuklia

0
419

Tanzania imesaini mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia, na kuifanya kuwa miongoni mwa nchi 60 zilizosaini na 32 zilizoridhia mkataba huo Duniani.

Utiaji saini wa mkataba huo umefanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, kando ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York nchini Marekani.

Akizungumza mara baada ya kutia saini mkataba huo, Profesa Kabudi amesema kuwa, kwa kusaini mkataba huo Tanzania inaunga mkono jitihada zote za kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia, ikiwa ni sehemu ya kuufanya ulimwengu kuwa mahali salama pa kuishi.

Hata hivyo Profesa Kabudi amesema kuwa, Tanzania inaunga mkono matumizi ya amani ya nyuklia.