Tanzania yafanya vizuri katika sekta ya Utalii

0
245

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amewapongeza viongozi wa Wizara ya Maliasili ya Utalii kwa kazi nzuri wanayofanya katika kuboresha Sekta ya Utalii nchini.

Balozi Kijazi ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam, wakati akifungua onesho la Kiswahili la Utalii la Kimataifa (SITE) kwa mwaka 2019, onesho linalohudhuriwa na Wadau wa Utalii kutoka Mataifa mbalimbali.

Amesema kuwa, Wizara ya Maliasili na Utalii imeiwezesha Tanzania kukua katika Sekta ya Utalii kwa asilimia 13 katika kipindi cha mwaka 2018 na kuzidi wastani wa ukuaji wa utalii Duniani ambao ulikua ni asilimia Sita.

Balozi Kijazi ameongeza kuwa, katika mwaka huo wa 2018, Sekta ya Utalii nchini ilichangia Dola Milioni 2.4 za Kimarekani katika fedha za kigeni, fedha ambazo zilikua ni Robo ya fedha hizo za kigeni.

Amewataka Wadau wa Utalii nchini kutumia Washiriki 500 wa onesho hilo kutoka Mataifa mbalimbali, kutangaza vivutio vya utalii nchini ili nao waende wakavitangaze vivutio hivyo katika nchi zao.