Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Desemba mwaka 2019 umebaki kuwa asilimia 3.8 kama ilivyokuwa kwa mwezi uliotangulia Novemba 2019
Akizungumza Jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa Sensa za Watu na Takwimu za jamii wa ofisi ya takwimu ya taifa – NBS, Ruth Minja amesema hali hiyo imetokana na kutokuwa na mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma
Aidha Minja amesema bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Disemba 2019 zimeongezeka bila kuathiri mfumuko wa bei huku katika nchi ya Kenya mfumuko wa bei umepanda hadi 5.82 na Uganda umepanda hadi kufikia asilimia 3.6