Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amesema mtu yeyote atakayepata virusi vya Corona nchini atatibiwa katika maeneo yaliyotengwa yaliyopo mkoani Kilimanjaro, Dar es Salaam na Mwanza.
“Kutokana na mwenendo na kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huu wa mapafu kipindi hiki, wizara inashauri kusubiri na kuepuka safari zisizo za lazima kwenda maeneo yaliyoathirika na inapolazimu kusafiri basi wapate maelezo ya kitaalamu kabla ya kuondoka nchini.
“Mpaka sasa Tanzania haina mgonjwa wala anayehisiwa kuwa na ugonjwa wa homa ya mapafu (Corona). Hata hivyo, kutokana na muingiliano uliopo kibiashara na kijamii kati ya Tanzania na nchi za Asia ikiwemo China, nchi yetu inakuwa katika hatari ya ugonjwa huo,” amesema Mwalimu.