Tanzania na Uingereza kuboresha zao la ngozi

0
197

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ametembelea taasisi inayojishughulisha na teknolojia na ubunifu wa mazao yatokanayo na ngozi ya Chuo Kikuu cha Northampton nchini Uingereza.

Akiwa chuoni hapo Waziri Mkenda amezungumza na uongozi wa juu wa chuo hicho na kufikia makubaliano maalum ya kuanza kubadilishana uzoefu kwa watumishi wa chuo hicho na taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) na kuanza kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa kitanzania katika eneo hilo.

Profesa Mkenda ameeleza kufurahishwa na wanachuo wawili wa kitanzania William Lohay na Azaria Chongeri wanaosoma chuoni hapo ambao ni watumishi wa DIT Mwanza ambayo imejikita kwenye tenolojia hiyo ya mazao ya ngozi .

Waziri Mkenda yuko nchini Uingezera ambapo anahudhuria kongamano la mwaka la Kimataifa la Elimu.