Tanzania na Uganda zaanza ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme Mto Kagera

0
241
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Bw. Geoffrey Mwambe kuhusu Maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa kufua umeme wa Kikagati-Murongo uliopo kwenye mto Kagera mpakani mwa Tanzania na Uganda unayotekelezwa na Nchi hizo kwa kutumia maji ya mto Kagera,Mradi huo unajengwa kwa Dola Milioni 90

Serikali za Tanzania na Uganda zinatekeleza ujenzi wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kufua umeme wa maji wa Kikagati-Murongo, uliopo kwenye mto Kagera mpakani mwa nchi hizo mbili utakaozalisha megawatts 14.

Inakadiriwa kuwa kila nchi itapata megawatts saba kati ya hizo 14 zitakazozalishwa mara baada ya Mradi huo kukamilika.

Mradi huo wa umeme wa unajengwa na kampuni ya kikandarasi ya PAC ya Italia unasimamiwa na kampuni Binafsi ya Uganda ya Kikagati-Murongo hydropower project ambayo ndio mjenzi wa Mradi huo ulioanza Mwezi Mei 2018 na kutarajia kukamilika Mei 2021 kwa gharama dola Milioni 90.

Ujenzi wa Mradi huo ni makubaliano ya nchi mbili za Tanzania na Uganda ya matumizi bora ya maji ya mto Kagera ambao upo mpakani mwa nchi hizo.

Bw.Geoffrey Mwambe ametembelea eneo la Ujenzi wa Mradi huo ili kukagua Maendeleo ya Ujenzi wake na kutaka maazimio ya Ujenzi wa Mradi huo ya asilimia 50 kila upande wa nchi hizo mbili za Tanzania na Uganda yazingatiwe.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti alisema kukamilika kwa Mradi huo kutasaidia kupatikana kwa umeme wa uhakika mkoani kwake.

Mhandisi Mshauri wa Mradi huo kutoka Kampuni ya nguvu za Nishati ya Geni Mhandisi Dkt Juliana Pallangyo alisema watasimamia ipasavyo ili kufanikisha Ujenzi wa Mradi huo na kuongeza kuwa kila nchi itanufaika katika kila hatua za Ujenzi na uendelezaji wa Mradi huo.

Mradi huo wa Kikagati-Murongo unajengwa kwenye Wilaya za Kyerwa Mkoani Kagera Tanzania na Wilaya ya Isingilo Nchini Uganda.