Tanzania na SADC – 2019

0
158

TANZANIA inatazamwa kuwa kiigizo chema na kuaminiwa kama daraja imara litalosaidia kuvusha ajenda ya uchumi na maendeleo ya viwanda kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika -SADC.

Kauli hiyo imetolewa jijini DSM na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya SADC, Dkt. STERGOMENA TAX, wakati wa mahojiano maalum na TBC ambapo amesema mwendo wa SADC kufikia maendeleo ya viwanda utachagizwa vyema na Uenyekiti wa TANZANIA chini ya Rais Dkt. JOHN MAGUFULI.