Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara uliojengeka kwa muda mrefu baina yake na Oman.
Rais Samia ameyasema hayo nchini Oman wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Oman, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini humo.
Akiwa nchini Oman Rais Samia Suluhu Hassan pia ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano katika sekta mbalimbali.
Amewakaribisha wawekezaji wa Oman kuwekeza Tanzania kwenye sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na utalii, kilimo, uvuvi, madini na ufugaji.
Kwa mujibu wa Rais Samia Suluhu Hassan, serikali inaendelea kurekebisha sheria na makosa yaliyojitokeza katika sekta ya uwekezeji na kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya uwekezaji nchini.