Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Namibia, – Netumbo Nandi-Ndaitwah wamesaini makubaliano ya pamoja kati ya Tanzania na Namibia.
Profesa Kabudi aliongozana na Rais John Magufuli nchini Namibia alipokwenda kufanya ziara rasmi ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais Hage Geingob wa nchi hiyo .