Tanzania na Msumbiji kuendeleza uhusiano

0
165

Rais Dkt John Magufuli amesema Tanzania itaendeleza uhusiano wake na Msumbiji, kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Dkt Magufuli ametoa kauli hiyo wilayani Chato mkoani Geita, akiwa na Rais wa Msumbiji, -Filipe Nyusi ambaye amefanya ziara hapa nchini.

Amesema Raia wa Tanzania na Msumbiji ni ndugu wa muda mrefu, hivyo ni muhimu kwa undugu huo ukaendelezwa.

Rais Magufuli amemshukuru Rais Nyusi kwa kufanya ziara hapa nchini, na kwa nchi yake kuwa rafiki mwema kwa Tanzania.

Amewataka Wananchi wa Msumbiji kuendelea kufanya biashara na wenzao wa Tanzana na kulinda usalama wa nchi yao.

Kwa upande wake Rais huyo wa Msumbiji amewashukuru Watanzania kwa mapokezi mazuri aliyoyapata wakati wa ziara yake hapa nchini.

Amempongeza Rais Magufuli kwa ushindi alioupata katika uchaguzi mkuu uliopita, na pia kwa Watanzania wote kwa utulivu waliouonesha kabla na baada ya uchaguzi huo.