Ili kuhakikisha vizazi vijavyo vinajua mpaka wa kimataifa wa Tanzania na Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan na Rais William Ruto wa Kenya wamekubaliana kufanya mapitio ya mpaka wa nchi hizo mbili.
Makubaliano hayo yamefikiwa leo katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya Rais Ruto hapa nchini.
“Ingawa kiutamaduni, kidamu hatuna mipaka lakini tuna mipaka ya kiutawala, wajue watoto wetu mipaka imepita wapi. Kazi hii ilishafanywa vizuri na sasa wataalamu wetu wakakae waone uwezo wa kuendesha zoezi hili awamu ya pili.” amesema Rais Samia Suluhu Hassan