Tanzania na China kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo

0
307

Serikali ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa China Leo zimesaini makubaliano ya kushirikiana kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo baina ya nchi hizo mbili ikiwa ni katika mkakati wa kuimarisha uhusiano uliodumu kwa muda mrefu kati ya nchi hizo.

Akizungumza Leo Jijini Dar es salaam wakati wa kusaini makubaliano hayo yaliyohudhuriwa na Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke na Naibu Spika wa Bunge la watu watu wa China Wang Chen,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa makubailiano hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano kati ya Taasisi binafsi za Tanzania na Taasisi binafsi za China kwenye utendaji kazi wa kila siku.

Aidha Spika Ndugai ameongeza kuwa makubaliano ni katika utekelezaji wa Mkakati ulioasisiwa na Rais wa Jamhuri ya watu wa China Xi Jinhping wa kusaidia nchi za Afrika kuweza kufikia malengo yake hivyo amesema Tanzania itanufaika kupitia makubaliano hayo.

Kwa upande wao Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke na Naibu Spika wa Bunge la watu wa China Wang Chen wamesema lengo la nchi ya China ni kuhakikisha nchi marafiki zinafanikiwa kupata maendeleo ya haraka pamoja na kuboresha maisha ya wananchi kupitia uboreshwaji wa huduma muhimu za jamii.