Tanzania na Barrick Gold waanzisha Kampuni ya Ubia

0
313

Serikali ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold , wameanzisha kampuni ya ubia inayojulikana kama Twiga  Minerals Corporation.

Taarifa za kuanzishwa kwa Kampuni hiyo zimetangazwa mbele ya Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi.

Profesa Kabudi amesema kuwa katika ubia huo, Kampuni ya Barrick Gold itakua na asilimia 84 na Serikali ya Tanzania asilimia 16.

Makao Makuu ya  Twiga Minerals Corporation yatakua jijini Mwanza.

Mkutano huo wa Profesa Kabudi na Waandishi wa habari pia ulihudhuriwa na uongozi wa juu wa Kampuni ya Barrick Gold.