Tanzania na Angola kuimarisha uhusiano

0
106

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, amefanya mazungumzo Balozi wa Angola nchini Sandro De Oliveira.

Mazungumzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma, ambapo Balozi huyo aliongozana na Mwakilishi wa Chama Tawala cha Angola (MPLA) Antonio Lobito.

Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Angola, pamoja na vyama vya ukombozi vya CCM na MPLA uliojengwa na waasisi wa mataifa hayo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Agustino Netho.

Aidha Balozi Sandro De Oliveira amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake wenye maono, na wenye kuwajali Watanzania katika kufikia maendeleo ya kweli.