Rais Samia Suluhu Hassan emeongoza mkutano wa maandalizi ya Foramu ya Masuala ya Chakula na Kilimo Afrika (AGRF) utakaofanyika Septemba 5 hadi 8 Mwaka huu.
Mkutano wa maandalizi ya mkutano huo mkubwa unafanyikia jijini Dar es Salaam ukijumuisha viongozi mbalimbali wa Mataifa ya Afrika hasa Sekta za Kilimo na Chakula
Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na hatua kubwa za kimageuzi ambazo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imezichukua tangu alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita.
AGRF ni jukwaa kuu la kuendeleza ajenda ya kilimo na mifumo ya chakula ambapo msisitizo utawekwa kwa vijana na wanawake kama msingi wa mfumo endelevu wa chakula barani Afrika.
Hatua hizo ni pamoja na kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo mara nne kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Serikali ya Tanzania pia imekuwa ikitekeleza mpango wa kilimo unaojulikana kama Ajenda 10/30 wenye lengo la kufanya kilimo kiwe cha biashara na kikue kwa wastani wa asilimia 10 kwa mwaka ifikapo 2030.