Tanzania kuuza umeme wake kwenye nchi za SADC

0
310
Kamishna wa Nishati Mhandisi Innocent Luoga

Serikali ya Tanzania inatarajia kuuza nishati ya umeme wa ziada kwa nchi wanachama wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika – SADC, pale utakapokamilika mradi mkubwa wa kufua umeme katika bonde la mto rufiji unaotarajiwa kuzalisha megawat 2115.

Hayo yameelezwa  na kamishna wa umeme na nishati jadidifu wa wizara ya nishati, mhandisi INNOCENT LUOGA  wakati akikagua banda la TANESCO katika maonesho ya NNE ya wiki ya viwanda ya SADC yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa julius nyerere.

Tanzania inazalisha nishati ya umeme kupitia vyanzo mbalimbali ambapo matumizi ni  wastani wa  megawati 1200 hadi 1400 , ukilingansiha za uzalishaji wa megawati 1600 kwa sasa. Mkakati kabambe wa serikali wa mradi wa kufua umeme katika bonde la mto RUFIJI ni kuzalisha megawati 2115. Mara baada ya kutosheleza mahitaji ya nchi. Umeme huo utauzwa kwa nchi za SADC na nyingine za Africa.

Kamishna wa umeme na nishati jadidifu wa wizara ya nishati, mhandisi INNOCENT LUOGA   amesema miundombinu ya  umeme ya kuzifikia nchi jirani utakamilika mwaka 2021.