Tanzania kupokea ugeni kutoka Uingereza

0
247

 
Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, – James Duddrige anatarajiwa kuwasili nchini hapo kesho kwa ziara ya siku mbili, yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Uingereza.

Akiwa hapa nchini, pamoja na mambo mengine Waziri Duddrige anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan na baadae atakutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi.

Akizungumza mkoani Dar es salaam kuhusu ujio wa Waziri huyo wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika , Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema Uingereza ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kuwekeza katika sekta ya uwekezaji na biashara nchini,  hivyo ujio wake ni fursa ya kuangalia maeneo muhimu ya kushirikiana na kufanya biashara baina ya nchi hizo mbili.