Tanzania kuongeza ubora wa filamu

0
330

Bodi ya filamu nchini imetoa ahadi kwa Watanzania kuboresha sekta ya filamu kwa kuandaa filamu bora zenye viwango na maudhui mazuri katika jamii.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu (TFB), Dkt. Kiago Kilonzo amesema filamu za Kitanzania zitaanza kuonyeshwa kwenye majumba ya sinema zikiwa na kiwango na ubora wa hali ya juu huku waandaaji wa filamu na wasanii wakiunga mkono juhudi hizo.

Bodi hiyo imekutana na wasanii pamoja na waandaaji wa filamu kujadili mbinu mbalimbali zitakazosaidia kufanikisha maboresho hayo.