Tanzania kukabiliana na changamoto soko la ajira

0
143

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, vijana na Watu wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akihututubia katika Mkutano Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani, ambapo ametoa salamu za Rais Samia Suluhu Hasan na kueleza juhudi zinazofanywa na Rais wa Tanzania katika kupambana na madhara ya UVIKO -19 katika Soko la Ajira.

Aidha, Waziri Ndalichako amelipongeza Shirika la Kazi Duniani kwa namna lilivyojipanga kusaidia nchi zinazoendelea katika bajeti zijazo na kuonesha utayari wa Tanzania kushirikiana na shirika hilo katika kutatua changamoto za soko la ajira hususani kuzalisha fursa za ajira kwa vijana, kuongeza wigo wa hifadhi ya jamii, kusimamia viwango vya kazi na kuimarisha uhuru wa majadiliano kati ya waajiri na wafanyakazi.

 Miongoni mwa juhudi alizozijata kufanywa na serikali ya Tanzania katika kutatua changamoto ya soko la ajira ni pamoja na kuanzisha na kutekeleza programu ya taifa ya kukuza ujuzi ambayo imewezesha vijana walio katika mazingira magumu wakiwemo wenye ulemavu kupata fursa ya mafunzo ya ujuzi wa kufanya kazi, kusimamia uanzishwaji wa mabaraza ya wafanyakazi, kusimamia kaguzi za kazi sehemu za kazi.

Ametaja jitihada nyingine kuwa ni pamoja na kuwezesha Bodi ya Kima cha Chini cha Mishahara kwa Sekta ya Umma na Binafsi na Maboresho katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii na kujali maslahi ya wafanyakazi.